• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu katibu mkuu wa UN atoa mwito wa kuwalinda raia kwenye eneo lisilo la kijeshi la Idlib nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-09-19 10:10:32

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya kibinadamu Bw. Mark Lowcock jana alitoa mwito wa kuwalinda raia kwenye eneo lisilo la kijeshi la Idlib nchini Syria.

    Bw. Lowcock ameliambia Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kamba bila kujali wako ndani au nje ya eneo hilo, raia lazima waruhusiwe kuondoka na kwenda mahali pengine kama wakitaka kuondoka.

    Bw. Lowcock amesema hayo wakati alipozungumzia makubaliano kati ya rais Vladimir Putin wa Russia na rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki kuhusu kuanzisha eneo lisilo la kijeshi huko Idlib.

    Amepongeza makubaliano hayo na kusema kama yakitekelezwa kwa msingi wa pande zote kuheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu, yataondoa msiba ulioonywa na Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako