• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Rais wa FIFA apinga Barcelona na Girona kupigwa Marekani

    (GMT+08:00) 2018-09-19 10:17:47

    Rais wa shirikisho la soka duniani (FIFA) Gianni Infantino amepinga mpango wa kuchezea mechi za ligi kuu Hispania nchini Marekani ukiwemo mchezo wa kwanza baina ya Girona na Barcelona.

    Infantino amesema ili uamuzi huo wa La Liga uweze kufanya kazi ni lazima mashirikisho ya soka ya Hispania na Marekani yaidhinishe, sawa na shirikisho la soka ulaya (UEFA), ridhaa nyingine itoke shirikisho la vyama vya soka vya Amerika kaskazini na kati (CONCACAF) pamoja na FIFA wenyewe.

    Katika siku za hivi karibuni kuna taarifa zinazoeleza kuwa mechi kati ya Girona na Barcelona itachezwa uwanja wa Hard Rock mjini Miami januari 26 mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako