• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi wa China atoa barua ya pongezi kwa shughuli ya siku ya kimataifa ya amani

    (GMT+08:00) 2018-09-19 13:33:02

    Rais Xi Jinping wa China ametoa barua ya pongezi kwa shughuli ya kumbukumbu ya siku ya kimataifa ya amani ya mwaka 2018.

    Rais Xi ametoa pongezi kwa kufanyika kwa shughuli hiyo kwa niaba ya chama cha kikomunisti cha China, serikali ya China na watu wake, huku akiwakaribisha wageni kutoka nchi mbalimbali, wajumbe wa mashirika ya amani ya kiraia na mashirika ya washauri bingwa na wengine kutoka jamii mbalimbali kushiriki kwenye shughuli hiyo.

    Rais Xi amesema, amani siku zote ni matarajio ya pamoja ya jamii ya binadamu. Hivi sasa, amani na maendeleo yamekuwa kaulimbiu ya zama hiyo, lakini tishio la usalama linalozikabili nchi mbalimbali linazidi kuongezeka, na tishio la vita haliwezi kuondolewa. Taifa la China linapenda amani, na watu wake wanajua thamani ya juu ya amani. China itaendelea kushika njia ya kujiendeleza kwa amani, ambayo siku zote itakuwa mjenzi wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya ulimwengu na mlinzi wa utaratibu wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako