• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Rais Kenyatta aongeza gharama za matumizi ya pesa kwa njia ya simu kwa 66%

    (GMT+08:00) 2018-09-19 18:52:54
    Gharama za utumaji pesa kwa njia ya simu kama vie M-Pesa zitaongezeka zaidi baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutoa pendekezo la kuongeza ushuru wa huduma hiyo kutoka asilimia 12 hadi asilimia 20.

    Rais Kenyatta analenga bidhaa kama utumaji pesa kwa njia ya simu,ambayo inatumiwa saa na wakenya,kama njia mojawapo ya kutandaza mzigo wa ushuru.

    Alisema ushuru unaotozwa kwa utumaji pesa kwa benki,mawakala wa utumaji pesa,na watoa huduma za fedha wengine,utakuwa asilimia 20.

    Mabadiliko hay yamekuja wiki kadhaa baada ya Waziri wa Fedha Henry Rotich kuongeza ushuru kwa asilimia 2 hadi asilimia 12 tarehe 1 Julai,na kufanya waendeshaji kuongeza gharama za utumaji pesa kwa njia ya simu.

    Tarehe 1 Julai,kampuni ya Safaricom iliongeza gharama za M-Pesa ambapo wale wanaofanya miamala mikubwa wakipata gharama za juu zaidi.

    Gharama za utoaji pesa wa kiwango cha kati ya Sh501 na Sh2,500 kutoka kwa wakala wa M-Pesa ziliongezeka kwa Sh1 na kugharimu Sh28 kutoka Sh27 ilhali gharama za utoaji wa kati ya Sh2,501 na Sh3,500, ambao uligharimu Sh49 uliongezeka hadi Sh50.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako