• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Waagizaji bidhaa waonywa bidhaa kukaguliwa kabla ya kuingizwa nchini

    (GMT+08:00) 2018-09-19 18:53:14
    Waagizaji bidhaa ndogo kutoka nje na mawakala wa forodha mkoani Dar es Salaam,Tanzania wameshauriwa kuhakikisha bidhaa zinazoagizwa nje zinakaguliwa ubora wake kabla hazijaingizwa nchini kupitia mfumo unaojulikana kitaalamu kama Pre-Shipment/Export Verification of Conformity to Standards.

    Kwa lengo la kuepuka usumbufu,ushauri huo ulitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania,TBS,Dk Yusuf Ngenya,wakati wa semina ya siku moja kwa waagizaji wa bidhaa ndogo ndogo nje ya nchi na mawakala wa forodha.

    Alisema ili kudhibiti bidhaa zisizokuwa na viwango kutoka nje ya nchi,Sheria ya Viwango Namba 2 ya mwaka 2009 imeipa mamalaka Shirika hilo kufanya ukaguzi huko zilipo kabla ya kuingia nchini.

    Dk Ngenya alisema Shirika hilo limekuwa likifanya kazi ya ukaguzi nje kwa kutumia mawakala walioidhinishwa kwa lengo la kuwaondolea usumbufu wafanya biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako