• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa Rwanda umekua kwa asilima 6.7 katika robo ya pili ya mwaka

    (GMT+08:00) 2018-09-19 18:53:33
    Uchumi wa Rwanda umekua kwa asilimia 6.7 katika robo ya pili ya mwaka 2018.

    Hii ni kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa na Wizara ya Fedha NA Mipango ya kiuchumi ya nchi hiyo jana.

    Utendaji huo unaashiria ukuaji zaidi kutoka ukuaji wa asilimia 4 ulioandikishwa kipindi sawa na hicho mwaka jana.

    Katika robo ya pili ya mwaka 2018,pato la taifa (GDP) katika bei za sasa za soko,linakadiriwa kuwa Rwf2,000 bilioni, kutoka Rwf1, 869 bilioni katika robo ya pili ya mwaka 2017.

    Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu Rwanda,ambayo kwa pamoja na Wizara ya Fedha,ilitoa takwimu hizo,ukuaji huo chanya umechangiwa na ukuaji wa sekta tatu kuu za uchumi.

    Sekta hizo ni pamoja na kilimo,ambayo ilikua kwa asilimia 6,viwanda,iliyopta ukuaji wa asilimia 10,na huduma 5%.

    Waziri wa Fedha na mipango ya uchumi Dk Uzziel Ndagijimana alisema kuwa ukuaji wa uchumi unaashiria matumaini kwamba nchi hiyo itafikia malengo ya ukuaji wa asilimia 7.2 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako