Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya imesema ukaguzi katika mitandao ya simu ya Safaricom,Airtel,na Telkom umebaini kuwa taarifa kuhusu wateja haziko sahihi,na pia kuna kadi za simu ambazo hazijasajiliwa,na hivyo kusaidia katika vitendo vya uhalifu.
Makosa yaliyopatikana ni pamoja na kadi za simu ambazo zimesajiliwa mara mbili au zaidi chini taarifa za watu tofauti,kutowiana kwa nambari za usajili kwa kutumia pasipoti na vitambulisho vya raia wa kigeni na pia waendeshaji kukosa kuwadhibiti mawakala wao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |