• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanawake wa Sudan Kusini wapongeza makubaliano ya amani

    (GMT+08:00) 2018-09-20 09:18:04

    Wanawake wa Sudan Kusini wametoa wito kwa viongozi wa nchi hiyo kuonesha nia ya kisiasa ya kutekeleza makubaliano ya amani.

    Wito huo umetolewa kwenye matembezi ya amani ya kupongeza makubaliano ya amani yaliyosainiwa hivi karibuni, siku moja kabla ya siku ya kimataifa ya amani Septemba 21.

    Bibi Betty Sunday aliyeongoza matembezi hayo amesema huko Juba kuwa wanawake wakishirikiana na makundi mbalimbali ya kiraia, wanapongeza makubaliano ya amani yaliyosainiwa, na kuwataka rais Salva Kiir, kiongozi wa waasi Bw. Riek Machar na pande nyingine kuchukua hatua halisi kutekeleza makubaliano hayo.

    Bibi Sunday amewahimiza viongozi waliosaini makubaliano ya amani kuweka kando tofauti za kisiasa, na kutekeleza kihalisi makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako