• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mazingira barani Afrika kuhimiza uvumbuzi kutatua changamoto kwenye nchi zao

    (GMT+08:00) 2018-09-20 09:27:38

    Mawaziri wa mazingira wa nchi za Afrika wamemaliza mkutano wa siku tatu mjini Nairobi, na kuamua kuhimiza njia za uvumbuzi kwenye utatuzi wa maswala ya mazingira, ili kutekeleza hatua za kuhifadhi mazingira ya asili na changamoto nyingine zinazozikabili nchi zao.

    Mawaziri hao pia walikubaliana kuhimiza kujenga uwezo wa nguvu kazi ili kutimiza maendeleo endelevu barani Afrika. Waziri wa mazingira wa Morocco ambaye pia ni makamu mkuu wa baraza la mawaziri wa Afrika kuhusu mazingira AMCEN, Bw. Nezha El Ouafi, amesema wataanza kuwawezesha wavumbuzi, sekta binafsi, mashirika madogo na yenye ukubwa wa kati pamoja na taasisi za kiraia katika kutumia mbinu mpya kukabiliana na changamoto za mazingira.

    Mawaziri hao wamesisitiza kuwa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta bifasi, utakuwa na mchango mkubwa, katika kubadilisha sera za mazingira kuwa utekelezaji halisi kuhusu kufanikisha ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063, na ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako