• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watanzania wateuliwa na CAF kusimamia na kuchezesha mechi za kufuzu AFCON

    (GMT+08:00) 2018-09-20 09:38:34

    Shirikisho la mpira wa miguu barani Africa (CAF) limetaja waamuzi kutoka nchini Tanzania kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 Cameroon kati ya Seychelles na Afrika Kusini utakaochezwa uwanja wa Stade Linite Oktoba 16 mwaka huu.

    Kwenye mchezo huo mwamuzi wa kati atakua Mfaume Ali Nassoro akisaidiwa na mwamuzi namba 1 Ferdinand Chacha, mwamuzi msaidizi namba 2 Alli Kinduru na mwamuzi wa akiba Elly Sasii. Huku mtathmini waamuzi anatokea Uganda Ronnie Kalema na Kamishna wa mchezo anatokea France Yves, Jean-Baptiste Etheve.

    Pia shirikisho hilo, limemteua Bwana Ahmed Idd Mgoyi kuwa kamishna wa mchezo wa Kufuzu kucheza AFCON 2019 Cameroon, mchezo ambao utazikutanisha Malawi na Cameroon mchezo utakaochezwa Oktoba 16, mwaka huu uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre

    Naye Leslie Liunda ameteuliwa kuwa mtathmini waamuzi mchezo utakaowakutanisha Congo DR na Zimbabwe utakaochezwa Kinshasa Complexe Omni Sports Stade Des Martyrs Oktoba 13 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako