• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Teknolojia mpya za juu kuwanufaisha binadamu

    (GMT+08:00) 2018-09-20 16:44:49

    Hivi sasa jamii ya binadamu inafanya mapinduzi ya nne ya viwanda, haswa katika sekta za akili ya bandia, nishati safi, na teknolojia za roboti, upashanaji wa habari kwa njia ya Quantum, VR na viumbe. Je, ni vipi teknolojia mpya za hali ya juu zinaweza kuwanufaisha zaidi binadamu? Mikutano mwili ya kimataifa iliyofanyika hivi karibuni nchini China imetoa majibu.

    Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa akili ya bandia ulifanyika mjini Shanghai, China kuanzia tarehe 17 hadi 19. Tangu wanasayansi wa Marekani watoe jina la "akili ya bandia" kwa mara ya kwanza mwishoni mwa miaka ya 50 ya karne iliyopita, teknolojia ya akili ya bandia inabadilisha maisha ya watu kwa kina. Kwenye mkutano huo, watu waliona matumizi ya teknolojia hiyo katika mambo ya elimu, afya, fedha, biashara ya rejereja, mawasiliano ya barabarani na huduma, na pia walitambua kiwango cha maendeleo ya teknolojia ya bandia nchini China. ripoti iliyotolewa na mkutano huo inasema, hadi katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, China ilikuwa inashika nafsi ya pili kwa idadi ya kampuni za akili ya bandia.

    Aidha ripoti hiyo inasema, matumizi ya akili ya bandia bado yako katika kipindi cha mwanzo, ambapo asilimia 4 tu ya kampuni zimewekeza kwenye teknolojia hiyo. Kama teknolojia hiyo ikitumiwa kwa mapana, itakuwa injini mpya kwa maendeleo ya uchumi na jamii duniani. Ili kutimiza lengo hilo, mafungamano ya uchumi duniani yanapaswa kuhimizwa zaidi, huku nchi mbalimbali duniani zikitakiwa kufungua mlango na kuongeza ushirikiano wa kimataifa.

    Mkutano mwingine wa kimataifa ni mkutano wa mwaka 2018 wa majira ya joto wa Baraza la Davos, ambao pia umefuatilia mapinduzi ya nne ya viwanda. waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alipohutubia ufunguzi wa mkutano huo alitoa mapendekezo ya kulinda kithabiti utandawazi wa uchumi duniani, kuongeza ushirikishi wa maendeleo, na kuhimiza kuunganisha uvumbuzi na maendeleo, ili kukuza injini mpya ya maendeleo ya uchumi wa dunia katika mapinduzi ya nne ya viwanda.

    Kwa kweli, kauli mbiu ya mkutano huo inaendana kwa kina na mkakati unaotetelewa na China wa kuhimiza maendeleo kwa uvumbuzi. Katika mapinduzi ya nne ya viwanda, China imepiga hatua katika teknolojia mpya mbalimbali za kisasa. Hivi sasa teknolojia hizo zinachangia theluthi moja ya maendeleo ya uchumi wa China, na kuleta theluthi mbili za ajira mpya mijini, na pia zimeweka msingi kwa ajili ya mageuzi ya maendeleo ya uchumi wa China.

    Mikutano miwili ya kimataifa iliyofanyika nchini China yote imefuatilia namna ya kuzifanya teknolojia mpya za juu kuwanufaisha binadamu. Mapinduzi ya nne ya viwanda yameanza, na kutoa fursa sawa kwa watu wote. Endapo mafungamano ya uchumi duniani yataendelea kusonga mbele, kila mtu atahamasishwa kufanya uvumbuzi, na kunufaika na mapinduzi hayo kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako