• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la "kujenga njia yenye uvumbuzi ya Ukanda Mmoja na Njia Moja" lafanyika mjini Tianjin

    (GMT+08:00) 2018-09-20 16:52:42

    Kongamano la "kujenga njia yenye uvumbuzi ya Ukanda Mmoja na Njia Moja" ambalo ni sehemu muhimu ya mkutano wa mwaka 2018 wa Baraza la majira ya joto la Davos limefanyika leo mjini Tianjin.

    Mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. He Lifeng amesema kuwa, pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" limepata matokeo makubwa tangu miaka mitano iliyopita lilipotolewa, na China imesaini nyaraka za ushirikiano 150 na nchi na mashirika ya kimataifa husika. Amesema, uvumbuzi ni sehemu muhimu ya kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    "Tunaona kuna mambo mawili kuhusu uvumbuzi ambayo ni muhimu. Kwanza wazo la kujenga kwa pamoja Ukanda Mmoja na Njia Moja kwa kupitia uvumbuzi linahusu urafiki, udhati, manufaa na shirikishi. Pande zote zinaishi kwa amani, kufundishana, kunufaishana, na kutambua kuwa kanuni ya kujenga kwa pamoja Ukanda Mmoja na Njia Moja ni kujadiliana, kujenga kwa pamoja na kunufaishana. Watu wanafuatilia katika mawasiliano ya sera, vifaa, biashara, mambo ya fedha na utamaduni. Mawazo hayo ni mapya kati ya nchi na nchi. Kama haya yakihimizwa ndipo ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja yataendelezwa kwa utulivu. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako