• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wapongeza mafanikio ya mazungumzo kati ya viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2018-09-20 18:32:18

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amepongeza mafanikio yaliyopatikana katika mazungumzo ya tatu kati ya viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini.

    Bw. Guterres amesifu jitihada za kidiplomasia zilizotumika kufikia azimio la pamoja la Pyongyang na kuhimiza pande hizo mbili kuchukua hatua kujenga uaminifu wa kijeshi na kutimiza ahadi ya kufunga kiwanja kilichokuwa kikitumika kwa majaribio ya silaha za nyuklia chini ya uangalizi ya wataalam wa nchi husika.

    Pia ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushikamana zaidi kuunga mkono pande husika kutimiza amani endelevu katika peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako