Halmashauri ya mawasiliano ya Kenya imearifu ukaguzi mkuu uliofanywa kwa kampuni za Safaricom,Airtel na Telkom umebainisha kuna baadhi ya watumiaji wa simu hizo ambao hawasajiliwa.
Baadhi ya hitilafu zilizopatikana ni pamoja na simu kadi kupatikana na watumiaji zaidi ya wawili,mvurugano wa tofauti kati ya wamiliki wa simu hizo wanaotoka nje ya nchi ,pamoja na tofauti kati ya waendeshaji wa simu na maajenti.
Francis Wangusi amesema kufikia Ijumaa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya uhalifu wa aina yoyote wa simu za mkononi.
Faini ya laki moja aidha itatolewa kwa watakaopatikana kukikuka amri hii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |