• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wajasiriamali 5 kuiwakilisha Tanzania jukwaa la uwekezaji Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-20 19:50:02
    Wamiliki 5 wa viwanda vidogo na kati nchini wamechaguliwa kushiriki katika jukwaa uwekezaji linalotarajiwa kufanyika nchini Kenya ikiwa ni sehemu ya kutafuta njia sahihi za kuondokana na tatizo la lishe katika nchi za Afrika.

    Waliochaguliwa kuiwakilisha Tanzania ni wamiliki wa viwanda vya East Africa Fresh Fruits, Crop Bioscience, AFCO Investment, Health Maisha na Kibaigwa Flour ambavyo vinajihusisha na masuala ya kilimo na lishe.

    Hatua hiyo ni matokeo ya shirika la kimataifa katika masuala ya kukuza lishe (Global Alliance for Improved Nutrition(GAIN)) wakishirikiana na SUN Bussiness Network waliandaa mashindano ya ndani ya nchi kupata washindi watano watakaoiwakilisha Tanzania katika Jukwaa la wawekezaji Afrika ili kukuza viwanda vidogo na vya kati kwenye sekta ya lishe na kuwaandaa kuwa wawekezaji wakubwa.

    Kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Chakula (WFP) inaonyesha asilimia 34 ya watoto Tanzania wamedumaa kutokana na utapiamlo, huku wanawake wakiwa wahanga wa anaemia na tatizo la kuongezeka kwa uzito wa kupitiliza pamoja na unene linazidi kuongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako