• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina mengi ya kuifahamisha dunia kuhusu mageuzi na ufunguaji mlango

    (GMT+08:00) 2018-09-21 09:08:27

    Imefahamika kuwa China ina mambo mengi ya kuifahamisha dunia kuhusu sera yake ya mageuzi na ufunguaji mlango ya China. Wakiongea kwenye kongamano lililoandaliwa na ofisi ya habari ya baraza la serikali ya China linalohimiza kutengeneza vipindi vya televisheni kuhusu mageuzi na ufunguaji mlango China, waongozaji wamesema kuna mengi ambayo China inaweza kuiambia dunia.

    Mwongozaji mkuu wa studio za BBC Bw. Matthew Springford amesema katika miaka 40 iliyopita, mageuzi ya China na kasi ya mabadiliko vimeifanya China iwe na hadithi nyingi za kufurahisha.

    Mwongozaji aliyepata tuzo ya Academy, Malcom Clarke, aliyetengeneza filamu ya "Better Angels" mwaka 2016, amesema kuna mambo mengi ambayo dunia inataka kujua kuhusu maendeleo ya China. Ametoa mfano wake mwenyewe kuwa alipokuja China kwa mara ya kwanza kwenye miaka ya 80 kulikuwa na umaskini, lakini sasa mazingira ya umaskini yamepotea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako