• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa China afanya mazungumzo na wawakilishi wanaohudhuria mkutano wa Davos wa majira ya joto

    (GMT+08:00) 2018-09-21 09:08:52

    Waziri Mkuu wa China Bw. Li Keqiang amefanya mazungumzo na wawakilishi kutoka sekta za viwanda na biashara, fedha, jumuiya za washauri bingwa na vyombo vya habari wanaoshiriki kwenye mkutano wa Davos wa majira ya joto unaofanyika mjini Tianjin.

    Kwenye mazungumzo hayo yaliyoandaliwa na mwenyekiti mtendaji wa Baraza la uchumi la Davos Bw Klaus Schwab, Bw Li alijibu maswali kuhusu China kufungua sekta ya fedha, ulinzi wa haki miliki ya ujuzi, kupunguza kodi, uvumbuzi na mageuzi ya mfumo wa biashara wa dunia.

    Kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na wawakilishi zaidi ya 200 kutoka China, Ulaya, Japan na Marekani, Waziri Mkuu Li amesema China kufungua sekta ya fedha, kuna uhusiano wa karibu na hatua ya maendeleo, kiwango cha uchumi na uwezo wa usimamizi.

    Waziri Mkuu Li pia amezungumzia suala la kodi, na kusema kupunguza kodi na ada nyingine kutapunguza mzigo kwa makampuni na kuhimiza maendeleo yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako