• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inatathmini madhara ya hatua za ushuru za Marekani

    (GMT+08:00) 2018-09-21 09:09:12

    China inatathmini madhara yanayoweza kusababishwa na uamuzi wa Marekani kutoza ushuru wa nyongeza kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 200 za Kimarekani.

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw Gao Feng, amesema hadi sasa ni bidhaa za aina sita zilizotajwa kwenye orodha ya kutozwa ushuru huo, na makampuni ya kigeni yanakadiriwa kuwa nusu ya makampuni yatakayoathiriwa.

    Bw. Gao amesema hatua za upande mmoja za kujilinda kibiashara za Marekani, sio tu zinaathiri makampuni na wateja wa China na Marekani, bali pia zinaathiri usalama wa mfumo wa uzalishaji duniani. Pia amesema kutokana na hatua hiyo ya Marekani, baadhi ya makampuni ya kigeni yaliyowekeza nchini China, yameanza kuangalia zaidi soko la ndani la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako