• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini kutumia umeme kutoka nchi jirani ili kuongeza ukuaji wake

    (GMT+08:00) 2018-09-21 09:56:27

    Waziri wa mabwawa na umeme wa Sudan Kusini Bw. Dhieu Mathok amesema nchi hiyo itaunganisha umeme kutoka nchi jirani na kujenga mabwawa ya ziada ya kuzalisha umeme, ili kuongeza maendeleo na ukuaji wake.

    Bw. Mathok amesema serikali itatekeleza mikataba ya kuunganishwa na umeme iliyosainiwa kati yake na Ethiopia na Uganda, kufanya kazi na China kufadhili ujenzi wa bwawa la Fula la megawatt 1,080 lililoko katika mji wa Nimule ulioko mpakani na Uganda. Ametangaza kuwa Rais Salva Kiir alifanya ziara ya hivi karibuni nchini China wakati wa mkutano wa FOCAC na kusaini makubaliano ya kuendeleza sekta ya nishati kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako