• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM aona kuwa utaratibu wa pande nyingi inakabiliwa na changamoto

    (GMT+08:00) 2018-09-21 10:14:12

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametaka Makubaliano yaliyofikiwa kati ya Uturuki na Russia yatekelezwe, ili kuokoa mkoa wa Idlib, Syria.

    Hayo yanajiri kutokana na hofu kuwa shambulizi la serikali ya Syria lililoungwa mkono na Russia dhidi ya mkoa unaokaliwa na waasi wa Idlib, linaweza kusababisha matukio ya umwagaji damu dhidi ya wakazi milioni tatu wa mkoa huo.

    Bw. Guterres amesema utaratibu wa pande nyingi sasa unakabiliwa na changamoto mbalimbali wakati unapohitajika, na pia amesisitiza umuhimu wa utaratibu wa dunia unaofuata msingi wa kanuni, na Umoja wa Mataifa ambao ni baraza linalostahiki la ushirikiano wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako