• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la pili la matangazo ya kimataifa kuhusu "Njia ya hariri baharini ya karne ya 21" lafanyika nchini China

    (GMT+08:00) 2018-09-21 10:28:26

    Kongamano la pili la matangazo ya kimataifa kuhusu "Njia ya hariri baharini ya karne ya 21" linaloandaliwa na Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha China na serikali ya mkoa wa Guangdong limefanyika mjini Zhuhai, kusini mwa China. Wataalamu, wasomi na viongozi wa vyombo vya habari wamefanya mawasiliano ya kina kuhusu hatua na mafanikio ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari. Waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa Bw. Jean-Pierre Raffarin anayehudhuria kongamano hilo, amepongeza pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Anasema,

    "Tunatakiwa kuanzisha ushirikiano zaidi katika maeneo ya 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'. Tutakuwa na miradi mingi katika muungano wa vifaa, urahisishaji wa biashara na mzunguko wa fedha. Kuhusi miradi ya 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', nchi zote husika zinazungumzia ushirikiano na kujenga mustakabali mpya. Hii ni muhimu sana kwa nchi za Ulaya."

    Naibu mkuu wa Radio China Kimataifa Bw. Hu Bangsheng alipozungumzia jinsi ya kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari chini ya utaratibu wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", amesema kuwa vyombo vya habari vinatakiwa kujenga mfumo wa mawasiliano ya moja kwa moja, kuheshimu kanuni za kimataifa za vyombo vya habari, na kutangaza kwenye maeneo ya wasikilizaji ili kutimiza lengo la utangazaji wenye uhalisi na maelewano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako