• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ligi kuu Tanzania Bara, Simba yarandwa na Mbao, African Lyon yapeta

    (GMT+08:00) 2018-09-21 10:39:57

    Mabingwa watetezi wa Tanzania Bara Simba SC jana wamepoteza mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji Mbao FC uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

    Kwa ushindi huo, Mbao FC wamepanda kileleni mwa ligi hiyo, wakifikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi tano, wakiwazidi kwa pointi moja Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu.

    Simba SC wanabaki na pointi zao saba baada ya kucheza mechi nne, wakishinda mbili dhidi ya timu za Mbeya, Tanzania Prisons 1-0 na Mbeya City 2-0, sare moja 0-0 na Ndanda FC na kipigo cha Mbao FC.

    Nayo African Lyon imepata ushindi wa kwanza wa ligi hiyo kwa kuilaza Singida United 3-2 mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako