• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OLIMPIKI 2032: Korea Kusini na Kaskazini zakubaliana kuandaa michuano ya Olimpiki ya mwaka 2032

    (GMT+08:00) 2018-09-21 10:41:15

    Korea Kusini na Korea Kaskazini zimekubaliana kutuma ombi la pamoja la kuandaa michuano ya Olimpiki ya mwaka 2032. Hatua hiyo imefikiwa baada ya mkutano wa pamoja baina ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un na rais wa Korea Kusini Moon Jae In.

    Mataifa hayo mawili kwa pamoja yaliandaa mashindano ya Asia, ikiwa ni ishara ya kuimarisha uhusiano baina yao. Hata hivyo ombi la Korea Kaskazini na Kusini linatazamiwa kupata upinzani kutoka kwa mataifa ya Australia, China na Indonesia ambayo pia yananuia kuandaa mashindano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako