• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasema Korea Kaskazini inapaswa kuacha mpango wake wa nyuklia kwanza

    (GMT+08:00) 2018-09-21 17:15:33

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema, katika kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea, Korea Kaskazini inapaswa kuacha mpango wake wa nyuklia, la sivyo vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi hiyo vitaendelea.

    Msemaji wa wizara hiyo Heather Nauert amesema, mkutano kati ya viongozi wa Korea Kusini na Korea Kaskazini umesukuma mbele mchakato wa kutimiza Peninsula ya Korea isiyo na silaha za nyuklia, lakini Korea Kaskazini inapaswa kuondoa silaha za nyuklia kwanza, na kama haitafanya hivyo, mambo mengine hayawezi kujadiliwa.

    Pia amesema, vikwazo vya Marekani dhidi ya Korea Kaskazini vitaendelea, ili kutimiza lengo la kuifanya Korea Kaskazini kuondoa silaha za nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako