• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi 128 kutoka nchi mbalimbali watarajia kushiriki kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2018-09-21 17:38:13

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, viongozi 128 kutoka nchi mbalimbali watashiriki kwenye mkutano wa Baraza Kuu la 73 la Umoja wa Mataifa.

    Bw. Guterres amesema, hali hii inaonesha uaminifu wa jumuiya ya kimataifa kwa umoja huo ambao unachukua nafasi muhimu duniani, na utatumia fursa hiyo kuhimiza pande zote kutoa ahadi mpya kwa umoja huo. Pia ameeleza wasiwasi wake kuhusu mashambulizi dhidi ya mfumo wa pande mbalimbali.

    Habari zinasema, Bw. Guterres atashiriki kwenye mikutano mitatu muhimu ya suala la vijana, kutafuta fedha kwa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na operesheni za kulinda amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako