• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idara ya mashtaka ya WTO yakabiliwa na changamoto kubwa

    (GMT+08:00) 2018-09-21 18:40:02

    Jaji wa idara ya mashtaka ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) kutoka Mauritius Bw. Shree Baboo Servansing anakaribia kumaliza muda wake wa kazi, na idara hiyo itaweza kukwama, hivyo kulifanya Shirika hilo kukabiliwa na changamoto kubwa zaidi katika historia yake.

    Tarehe 28 mwezi uliopita Marekani ilikataa kumwongezea Servansing muhula wa pili wa kuwa jaji wa idara hiyo, ikimaanisha kuwa hadi kufikia tarehe 30 mwezi huu baada ya kuondoka kwa Servansing, idara hiyo itakuwa na majaji watatu tu, ambao ni wachache zaidi katika kushughulikia kesi ya mashtaka ya biashara.

    Wachambuzi wanasema, kuna mambo muhimu matatu katika kuhimiza mageuzi ya Shirika hilo, ambayo ni kuondoa vizuizi vya Marekani dhidi ya idara hiyo, kumaliza vitendo vya kujilinda kibiashara na vya upande mmoja, na kushikilia kanuni ya mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako