• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CRDP yageukia vicoba na Harusi

    (GMT+08:00) 2018-09-21 20:35:13

    Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya wizi wa fedha unaochangiwa na kukosekana kwa uaminifu kwa wanavikundi vya kujikwamua kiuchumi, Benki ya CRDB imebuni bidhaa tatu mpya ikiwamo akaunti ya Vicoba kupata akaunti kupitia simu ya mkononi ili kuondokana na changamoto zinazowakabili.

    Suluhisho hilo limebainishwa na meneja wa huduma za mtandao wa CRDB, Edith Metta alipotoa elimu kwa wanahabari kuhusiana na huduma hizo mpya kwa wateja.

    Katika siku za hivi karibuni, Metta alisema kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya vikundi kupoteza fedha kutokana na wizi au mmoja kukimbia nazo hali hiyo ilisababisha benki hiyo kuja na suluhisho.

    Alizitaji huduma hizo mpya kuwa ni akaunti ya kikundi, akaunti ya akiba na akaunti ya malipo.

    Kwa wanachama wa Vicoba alisema wanaweza kufungua akaunti ya pamoja kupitia simu za mkononi kisha kusajili jina la kikundi na kuanza kuweka na kutoa fedha bila makato yoyote.

    Metta alisema akaunti hiyo inahakikisha fedha zinakuwa salama na iwapo kuna udanganyifu umefanywa na yeyote wanakikundi wanajua mapema.

    Akaunti hiyo inatoa mwanya kwa wanachama kuanzia watatu hadi 3,000 wanaoweza kutunza mpaka Sh50 milioni, huku kukiwa na fursa ya kupata mikopo kwa kikundi kitakachokuwa na kumbukumbu nzuri za utunzaji fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako