• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenyatta asaini mswada wa fedha wa 2018

    (GMT+08:00) 2018-09-21 20:35:27

    Rais Uhuru Kenyatta ametia saini Mswada wa Fedha 2018 kuwa sheria. Hilo limejiri siku moja tu baada ya bunge la kitaifa kushuhudia vurumai kufuatia wabunge waliopinga mswada huo. Ulikuwa na mapendekezo ya Rais baada ya kukataa kuutia saini awali, ambapo wabunge walikuwa wamependekeza kuahirishwa kwa utozaji ushuru (VAT) wa asilimia 16 kwa mafuta.

    Kenyatta aliurejesha bungeni akitaka ufanyiwe marekebisho ambapo alishusha VAT hiyo kutoka asilimia 16 hadi 8. Mapendekezo mengine ni utozaji ushuru huduma za usambazaji wa pesa kwa njia ya simu, intaneti, mitandao, na huduma za benki. Rais pia alipendekeza kupunguzwa gharama ya matumizi kwa viongozi wakuu serikalini.

    Hata hivyo, shughuli ya upigaji kura kuupitisha ama kuurambisha sakafu ilishuhudiwa zogo Alhamisi idadi ya kamili kuuangusha ilipokosa kuafikiwa. Ni wabunge 215 pekee waliojitokeza katika kikao cha bunge kilichoongozwa na spika Justin Muturi.

    Baadhi ya wabunge waliopinga mapendekezo hayo walimyooshea kidole cha lawama spika Muturi, kiongozi wa wengi Aden Duale, kiongozi wa wachache John Mbadi na viongozi wa kamati mbalimbali bungeni, wakiwatuhumu kwamba walishawishi wabunge kuondoka kikao hicho ili kukosa kuafikia kigezo cha thuluthi mbili, sawa na wabunge 233 ili kuangusha mswada huo.

    Kwa upande Duale alisema ni wajibu wake kuhakikisha mikakati ya serikali imeafikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako