• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasifu uamuzi wa shirika la IAEA

    (GMT+08:00) 2018-09-22 16:38:14

    Shirika la nishati ya atomiki duniani IAEA jana limepitisha muswada wa uamuzi kuhusu kutoa uhakikisho na usimamizi kwa Korea Kaskazini. Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa huko Vienna Bw. Wang Qun amesema, uamuzi huo umehimiza utatuzi wa suala la nyuklia la peninsula ya Korea kwa njia ya kisiasa.

    Bw. Wang Qun amesema, tofauti na uamuzi wa zamani, uamuzi huo umekaribisha maendeleo yaliyopatikana kwenye suala la peninsula ya Korea, pia umeonyesha alama dhahiri ya kuunga mkono juhudi za kidiplomasia na kisiasa.

    Bw. Wang pia amesema, uamuzi huo pia umeihimiza jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za kujenga uaminifu, ili kusuluhisha hali ya wasiwasi kwenye peninsula ya Korea na kutimiza amani na ustawi wa peninsula hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako