• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifo kutokana na ajali ya kivuko nchini Tanzania vyafikia 156

    (GMT+08:00) 2018-09-22 16:41:06

    Rais wa Tanzania John Magufuli jana ametangaza siku nne za maombolezo kufuatia ajali ya kivuko iliyotokea katika ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu vilivyofikia 156 mpaka sasa.

    Katika kipindi hicho cha maombolezo, bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti na Rais Magufuli ameagiza watumishi wote wa kivuko hicho kushikiliwa na kuhojiwa kufuatia ajali hiyo, pamoja na kuwashikilia wakaguzi wa usalama kutoka mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa barabara na majini SUMATRA.

    Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kivuko hicho kilibeba mzigo kupita kiasi na kwamba kilikuwa kinaongozwa na mtu ambaye si nahodha aliyethibitishwa.

    Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemwagiza Waziri Mkuu na waziri wa Usafirishaji kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua.

    Mara ya mwisho kutokea ajali ya majini katika ziwa Victoria ilikuwa mwaka 1996 ambapo takribani watu 500 walipoteza maisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako