• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwakilishi maalumu wa rais Xi Jinping wa China ashiriki kwenye sherehe ya kuapishwa kwa rais wa Mali

    (GMT+08:00) 2018-09-23 16:05:45

    Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali jana kwenye Ikulu ya Mali amekutana na mwakilishi maalumu wa rais Xi Jinping wa China Bw. Zheng Jianbang ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China.

    Bw. Zheng amewasilisha pongezi za rais Xi Jinping kwa rais Keita. Amesema China inapenda kushirikiana na Mali kutumia fursa ya kutekeleza mafanikio ya mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mjini Beijing, kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye mawasiliano ya siasa, maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na amani na usalama.

    Rais Keita amemshukuru rais Xi Jinping kwa kumtuma mwakilishi maalumu kwenye sherehe yake ya kuapishwa, amesema Mali inatilia maanani na kukuza urafiki wa jadi kati yake na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako