• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yawashutumu mabalozi watatu kutoka nchi za Ulaya kwa kuhusika na shambulizi la jana

    (GMT+08:00) 2018-09-23 16:06:26

    Iran imewashutumu mabalozi kutoka nchi za Denmark, Uholanzi na Uingereza kwa madai kuwa walihusika na shambulizi wakati wa gwaride la kijeshi lililosababisha vifo vya watu 29 kusini mwa Iran jana.

    Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran IRNA, mabalozi wa nchi hizo tatu wanadaiwa kuwahifadhi baadhi ya magaidi waliohusika katika shambulizi la jana.

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Iran, Bw. Bahram Qasemi alinukuliwa akisema, haikubaliki kuona kwamba Umoja wa Ulaya hauchukui hatua dhidi ya vikundi vya kigaidi kwa kuwa havijafanya uhalifu kwenye ardhi ya Ulaya.

    Aidha Iran imeishutumu marekani na washirika wake kwa kushiriki shambulizi hilo ambalo baadaye kundi la IS lilijitangaza kuhusika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako