• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa Hamas, na Misri, wajadili makubaliano ya kumaliza migogoro wa ndani ya Palestina, na kusimamisha vita dhidi ya Israel

    (GMT+08:00) 2018-09-23 16:30:23

    Kundi la Hamas mapema jana limesema kiongozi wa kamati kuu ya uongozi wake Bw. Ismail Haneya amejadili na wasuluhishi waandamizi kuhusu majadiliano ya kusimamisha vita na Israel, na makubaliano ya kumaliza mgawanyiko kati ya wapalestina uliodumu kwa miaka 12.

    Katika taarifa hiyo, inaelezwa kuwa Haneya pamoja na ujumbe wa ngazi ya juu wa Misri walijadili masuala yanayohusu uhusiano wa kimkakati baina ya pande mbili, changamoto zinazoikumba Palestina na mchakato wa Israel wa kuitwaa Gaza.

    Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa kundi la Hamas linapenda kurudisha umoja baina ya wapalestina wakati huu ambapo kuna changamoto nyingi, hasa kuhusu masuala ya Jerusalem, wakimbizi na makazi.

    Hivyo ujumbe huo wa Misri unatarajiwa kuwasilisha maoni ya Hamas kwenye pande zote, kwa Israel na kwa Rais wa mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbas.

    Kwa miaka mingi sasa, Misri imekuwa msuluhishi kati ya Hamas na Abbas ili kumaliza mgogoro uliodumu kwa miaka 12, na imekuwa ikiitisha kusimamisha vita kati ya Palestina na Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako