• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Polisi wa Tanzania wakamata watuhumiwa wa ajali ya kivuko

  (GMT+08:00) 2018-09-24 08:45:53

  Waziri mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa amesema, polisi wamewakamata watu kadhaa wanaotuhumiwa kuhusika na ajali ya kivuko ambayo imesababisha vifo vya watu 224 ziwa Victoria.

  Akizungumza kwenye mazishi ya watu 9 wasiotambuliwa na familia kwenye kisiwa cha Ukara, Bw. Majaliwa pia amesema ataitangaza tume ya uchunguzi wa ajali hiyo mapema iwezekanavyo.

  Mazishi ya pamoja yamefanyika kwa baadhi ya miili ya watu waliofariki dunia kwenye ajali hiyo iliyotokea karibu na kisiwa cha Ukara mkoani Mwanza nchini Tanzania. Hadi sasa idadi ya watu waliopoteza maisha imetajwa kufikia 224.

  Rais John Magufuli ametangaza siku 4 za maombolezo ya ajali hiyo, na kutoa amri ya kuwakamata wakaguzi wa usalama wa mamlaka ya usafiri wa ardhi na baharini. George Njogopa na taarifa zaidi

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako