• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gofu, Uganda Open: Ronald Otile ashinda ubingwa

    (GMT+08:00) 2018-09-24 10:29:44

    Ronald Otile kutoka Uganda, jana ameshinda ubingwa wa mashindano ya mchezo wa gofu ya Uganda Open yaliyomalizika mjini Entebbe, licha ya kuwa alianza kwa kupiga mpira vibaya na kupoteza baadhi ya alama.

    Mshindi wa pili kwenye mashindano hayo alikuwa ni Edwin Mudanyi na John Karichu, wote kutoka Kenya na nafasi ya nne ikichukuliwa na Herman Mutebi kutoka Uganda.

    Hii ni mara ya pili kwa Otile kushinda taji hili la ubingwa kwa wachezaji wa ridhaa kwani mwaka 2015 na 2016 pia ndiye aliibuka bingwa.

    Kwa upande wa wawakilishi wa Tanzania, Victor Joseph kutoka Dar es Salaam alishinda nafasi ya tisa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako