• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikapu, Kombe la Dunia Wanawake: Nigeria yapata mtihani ili kufuzu robo fainali

    (GMT+08:00) 2018-09-24 10:34:08

    Timu ya taifa ya Nigeria ya mchezo wa mpira wa kikapu ya Wanawake, jana imepata ushindi muhimu kwenye hatua ya makundi ya mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini Hispania kwa kuifunga Uturuki kwa alama 74-68.

    Ushindi huo ulikuwa muhimu kwa Nigeria ambayo katika mechi yake ya kwanza ilipoteza dhidi ya Australia, na sasa itahitaji walau ushindi itakapocheza na Argentina ili iweze kufuzu hatua ya robo fainali.

    Timu nyingine kutoka Afrika ni Senegal, yenyewe tayari imefuzu hatua ya robo fainali kwa kuwa imeshinda mechi moja dhidi ya Latvia, lakini ikifungwa na Marekani, na faida kubwa ikipatikana baada ya Latvia kufungwa mechi zake zote mbili za hatua ya makundi.

    Katika mechi yake ya mwisho, Senegal itacheza na China kesho mjini San Cristobal huko Hispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako