• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi Kuu ya Italia: Ronaldo aendeleza makali yake, achangia ushindi wa Juve

    (GMT+08:00) 2018-09-24 10:38:45

    Kwa kile kilichoonekana kama kutokatishwa tamaa na kadi nyekundu aliyopata katikati ya juma lililopita, mchezaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo, jana amefanikiwa kufunga goli la kwanza la timu yake ya Juventus ilipocheza na timu ya Frosinone kwenye ligi kuu ya Italia.

    Kama haitoshi, Ronaldo pia alitoa pasi safi iliyozaa goli la pili lililofungwa na Federico Bernardeschi kunako dakika za lala salama.

    Hii ni mechi ya pili mfululizo kwa Ronaldo kufunga magoli, jambo lililomfanya afute presha aliyopata baada ya kutofunga kwenye mechi tatu za kwanza za ligi kuu ya Italia. Ronaldo pia alilimwa kadi nyekundu wakati wa mechi ya klabu bingwa jumatano iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako