• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa waraka kuhusu ukweli wa mgogoro wa kibiashara kati yake na Marekani na msimamo wake

    (GMT+08:00) 2018-09-24 13:36:11

    Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka kuhusu ukweli wa mgogoro wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani na msimamo wa China, unaolenga kuhimiza utatuzi mwafaka wa suala hilo.

    Waraka huo una sehemu sita ambazo ni pamoja na ushirikiano wa kusaidiana na kunufaishana wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, ukweli wa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, vitendo vya kujilinda kibiashara vya serikali ya Marekani, vitendo vya umwamba wa kibiashara vya serikali ya Marekani, athari mbaya ya vitendo visivyo sahihi vya serikali ya Marekani kwa maendeleo ya uchumi wa dunia na msimamo wa China.

    Waraka huo umesema China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani huku Marekani ikiwa ni nchi iliyoendelea zaidi duniani. Uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani una maana kubwa kwa nchi hizo mbili, pia una athari kubwa kwa utulivu na maendeleo ya uchumi wa dunia.

    Waraka huo umesema China na Marekani ziko katika vipindi tofauti vya maendeleo ya uchumi, na zina mifumo tofauti ya kiuchumi, kwa hiyo ni jambo la kawaida kwa nchi hizo kuwa na mivutano ya kiuchumi na kibiashara, lakini cha muhimu ni jinsi ya kuongeza hali ya kuaminiana, kuhimiza ushirikiano na kudhibiti tofauti. Kwa muda mrefu, serikali za nchi hizo mbili zinafuata kanuni za usawa, kuwa makini na kwenda sambamba na kuanzisha mifumo mbalimbali ya mawasiliano na majadiliano ikiwemo kamati ya pamoja ya biashara ya China na Marekani, mazungumzo ya uchumi wa kimkakati, mazungumzo ya mikakati na uchumi, mazungumzo ya kiuchumi ya pande zote, ambapo pande hizo mbili zimefanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati yao unakabiliana na vizuizi mbalimbali, kusonga mbele, kuwa msingi imara na kuhimiza uhusiano katika China na Marekani katika miongo karibu minne iliyopita.

    Waraka huo umesema tangu serikali ya Marekani ya awamu mpya iingie madarakani mwaka 2017, chini ya wito wa "Marekani kwanza", Marekani imepuuza kanuni za kimsingi za mawasiliano ya kimataifa za kuheshimiana na kujadiliana kwa usawa, kutekeleza sera ya upande mmoja, sera ya kujilinda na sera ya umwamba wa kiuchumi, na kutoa shutuma zisizo na msingi dhidi ya nchi na sehemu mbalimbali haswa kwa China, kufanya matishio ya kiuchumi kwa kuendelea kutoza ushuru wa nyongeza, na kuilazimisha China kukubali madai yake kwa njia ya kuweka mashinikizo yanayokaribia kuvuka mipaka.

    Waraka huo umesema katika kukabiliana na hali hiyo, China inasisitiza kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo na mazungumzo kwa ajili ya kulinda maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili na hali ya jumla ya utaratibu wa biashara ya dunia, kuangalia ufuatiliaji wa Marekani kwa uvumilivu na udhati wa kutosha, kushughulikia migogoro kwa msimamo mwafaka wa kuongeza maoni ya pamoja na kuweka kando tofauti, kukabiliana na taabu mbalimbali, kufanya mazungumzo zaidi na Marekani, kutoa mipango ya ufumbuzi inayofaa, na kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili. Hata hivyo, Marekani haifuati ahadi yake na kutoa changamoto mara kwa mara na kusababisha mvutano wa kiuchumi na kibiasahra kati yake na China uzidi kuwa mbaya ndani ya muda mfupi, na kuathiri vibaya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, ambao umejengwa kwa juhudi za miaka mingi na serikali za nchi hizo mbili na wananchi wake, pia imeleta tishio kubwa kwa utaratibu wa biashara wa pande nyingi na kanuni za biashara huria. Serikali ya China imetoa waraka huo ili kuweka bayana ukweli wa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, na kueleza kwa uwazi msimamo wa China kuhusu mgogoro wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, na kusukuma mbele utatuzi mwafaka wa mgogoro huo.

    Waraka huo umesema uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani unahusu maslahi ya watu wa nchi hizo mbili, pia unahusu amani, ustawi na utulivu wa dunia. ushirikiano ni chaguo pekee sahihi kwa nchi mbili, na manufaa kwa pande zote mbili yanaweza kufanya nchi hizo kuelekea kwenye siku nzuri za baadaye. Msimamo wa China ni wazi, wa kudumu na thabiti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako