• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa waahidi kufuata moyo wa Mandela

    (GMT+08:00) 2018-09-25 09:20:58

    Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limetoa heshima kwa Nelson Mandela kwa ahadi ya kujenga dunia yenye haki, amani na ustawi, na kufufua maadili yanayoshikiliwa na aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela.

    Kwenye mkutano wa kilele wa amani wa Nelson Mandela, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimepitisha uamuzi wa kwanza wa kikao cha 73 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa kuahidi kuonyesha hali ya kuaminiana, uvumilivu, maelewano na masikilizano katika uhusiano wao.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema Mandela alionyesha maadili ya juu zaidi uliyo nayo Umoja wa Mataifa, na alijitolea maisha yake kuhudumia jamii. Pia amekumbusha mabadiliko yaliyoletwa na Mandela kwa Afrika Kusini na hata kwa dunia nzima, akisema chini ya uongozi wake, Afrika Kusini ilipanua upatikanaji wa huduma za afya, elimu, nyumba, maji, usafi na umeme, na alikuwa na ushawishi mkubwa wa amani na demokrasia kwa nchi jirani za Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako