• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yazishutumu tena Marekani, Saudi Arabia na UAE kwa kuunga mkono shambulizi la kigaidi mjini Ahvaz

    (GMT+08:00) 2018-09-25 09:29:13

    Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amezishutumu tena Marekani, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kuunga mkono shambulizi la kigaidi lililotokea Jumamosi mjini Ahvaz, kusini magharibi mwa Iran, ambalo limesababisha vifo vya watu 25 na wengine 60 kujeruhiwa.

    Ayatollah Khamenei amesema habari husika zinaonyesha kuwa tukio hilo limefanywa na watu kutoka Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, ambao waliokolewa na Marekani walipozingirwa kwenye vita nchini Syria na Iraq. Ameongeza kuwa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zimewapa fedha magaidi hao.

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulizi hilo la kigaidi, na kusisitiza kuwa kuna haja ya kuwawajibisha waliohusika na shambulizi hilo na kuwafikisha mbele ya sheria. Limesisitiza tena kwamba nchi zote zinapaswa kukabiliana na matishio ya amani na usalama yanayoletwa na magaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako