• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inaweza kukabiliana na athari zinazotokana na ushuru wa nyongeza unaotozwa na Marekani dhidi ya bidhaa zake

    (GMT+08:00) 2018-09-25 12:41:14

    Naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Lian Weiliang amesema China ina uwezo wa kukabiliana na athari mbaya zinazotokana na ushuru wa nyongeza unaotozwa na Marekani dhidi ya bidhaa zake zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 kwa njia ya kupanua mahitaji ya ndani na kuhimiza maendeleo bora.

    Bw. Lian amesema mwaka jana ukubwa wa uchumi wa China ulifikia dola za kimarekani trilioni 12.7, huku thamani ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi ikiwa ilifikia trilioni 2.26, ambapo bilioni 200 ni asilimia 8.8 tu ya thamani hiyo. Aidha, China ina watu bilioni 1.4, idadi ambayo ni kubwa kuliko idadi ya watu wote wa nchi zilizoendelea kiuchumi, kipato cha wastani cha watu mmoja mmoja ni karibu dola za kimarekani elfu 9, pia kiwango cha matumizi kinaongezeka kidhahiri, kwa hiyo soko lina nguvu kubwa ambazo hazijatumiwa ipasavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako