• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema ni lini majadiliano ya ngazi ya juu ya kibiashara kati yake na Marekani kufanyika tena, hii itaamuliwa na nia ya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-09-25 12:41:35

    naibu waziri wa biashara wa China Wang Shouwen ambaye pia ni naibu mjumbe wa mazungumzo ya biashara ya kimataifa amesema ni lini majadiliano ya ngazi ya juu ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani yataanzishwa upya, hii itaamuliwa na nia ya Marekani.

    Wang amesema kutendeana kwa usawa na kuheshimana ni msingi wa majadiliano, lakini sasa majadiliano hayo yanakosa mazingira ya usawa wakati Marekani inachukua hatua ya kutoza kwa kiasi kikubwa ushuru wa nyongeza dhidi ya bidhaa za China. Aidha, udhati na kufuata ahadi pia ni muhimu kwa majadiliano. China na Marekani zimefanya majadiliano mara nne, ambayo yamepata maafikiano mengi, na hata zimetoa taarifa ya pamoja, lakini Marekani inapuuza makubaliano hayo na kuchukua hatua ya kukwamisha biashara na kufanya majadiliano yashindwa kuendelea kufanyika.

    Amesisitiza kuwa endapo Marekani ingekuwa na udhati na kufuata ahadi, majadiliano haya yangefanyika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako