• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Marekani na Korea Kusini wakubaliana kudumisha shinikizo kwa Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-09-25 17:00:52

    Rais Donald Trump wa Marekani na rais Moon Jae-in wa Korea Kusini wamekubaliana kudumisha shinikizo kwa Korea Kaskazini na kujadili mipango ya kufanya mkutano wa pili kati ya rais Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.

    Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Marekani imesema, rais Trump amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanywa ili kufikia lengo la pamoja la kuhakikisha Korea Kaskazini haina silaha za nyuklia.

    Rais Trump pia amepongeza mafanikio yaliyopatikana katika mkutano wa kilele kati ya rais Moon Jae-in wa Korea Kusini na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu mjini Pyongyang.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako