• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Iran wakutana

    (GMT+08:00) 2018-09-25 17:16:52

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif, kando ya mkutano wa Baraza Kuu la 73 la Umoja wa Mataifa unaofanyika mjini New York.

    Bw. Wang Yi amesema China inaiunga mkono Iran kulinda maslahi yake halali, kupinga umwamba wa upande wa mmoja, na kutetea kulinda makubaliano ya pande zote kuhusu suala la nyukilia la Iran.

    Bw. Zarif ameisifu China kwa kuonesha umuhimu mkubwa katika kulinda makubaliano ya pande zote kuhusu suala la nyukilia la Iran. Amesema Iran ina imani kuwa nchi nyingi duniani zitaendelea kuunga mkono makubaliano hayo, na kwamba Iran inapenda kudumisha mawasiliano na pande mbalimbali ikiwemo China kuhusu kulinda na kutekeleza makubaliano hayo, na kukabiliana kwa pamoja na hali ya hivi sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako