• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Shirika la ndege la Uganda lakosa fedha za kuanza upya

    (GMT+08:00) 2018-09-25 18:58:41

    Mipango ya shirika la ndege la Uganda la kuanza upya oparesheni zake mwezi Aprili 2019 zimesambaratika baada ya mfadhili wa Canada kujiondoa kwenye makubaliano akitaja sababau za kibiashara.

    Kampuni ya Cananda ya has Export Development Canada (EDC), ilikuwa imekubalia kulipa shirika hilo mkopo wa dola milioni 108 ili kununua ndege mpya lakini sasa limejiondoa kwa makubaliano.

    Chini ya makubaliano hayo Uganda ingenunua ndege nne aina ya Bombardier ili kuimarisha safari zake kwenye kanda ya Afrika Mashariki,'

    Maafisa wa wizara ya fedha ya Uganda wamesema wamepokea barua ya kusitisha makubaliano hayo kupitia kwa ubalozi wa Canada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako