• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wafanya biashara wa Uganda nchini Sudan Kusini waomba kulindwa

    (GMT+08:00) 2018-09-25 18:59:39

    Spika wa bunge la Uganda Rebecca Kadaga ameiomba serikali ya Sudan Kusini iwalinde wafanyabiashara wa Uganda walioko katika nchi hiyo jirani.

    Spika Kadaga amesema baadhi ya wafanyabiashara wa Uganda wanakabiliwa na hali ngumu kutoka kwa wenzao wa Sudan Kusini.

    Amesema katika mkutano wa hivi karibuni na wafanyabiashara wa Uganda mjini Juba, walimueleza kuwa wanatishiwa kufurushwa nchini humo ilhali wamewekeza fedha nyingi.

    Kadaga alikuwa mjini humo kuhudhuria mkutano wa maspika wa bunge za Afrika mashariki ambapo rais wa seneti la Rwanda Makuza, alitilia mkazo umuhimu wa biashara baiana ya nchi wanachama wa EAC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako