• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Watanzania kuuza mbaazi China

    (GMT+08:00) 2018-09-25 19:01:11

    Kampuni 45 za China zitaanza kununua mbaazi kutoka Tanzania.

    Wawekezaji hao wa China wamesema wapo tayari kununua bidhaa za mazao mengine kama kahawa, asali, tangawizi, mihogo, soya na chai yakiongezewa thamani.

    Taarifa hizo zimebainishwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) mwishoni mwa wiki hii.

    Mkurugenzi mkuu wa Tantrade, Edwin Retageruka amesema kampuni hizo zimeeleza utayari huo kwenye maonyesho ya China-Asean Expo (CAEXPO) yaliyofanyika Septemba 12 hadi 15 mwaka huu jijini Nannang, China ambako mashirika 23 ya umma na wafanyabiashara walihudhuria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako