• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Je, ni kweli Marekani imepata hasara katika biashara na China kama inavyodai?

    (GMT+08:00) 2018-09-25 20:08:28

    Mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani umedumu kwa miezi sita sasa, na Marekani siku zote inalalamikia kuwa imepata hasara kubwa katika biashara kati yake na China. Hicho pia kimekuwa kisingizio cha Marekani kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa kutoka wenzi wake wakuu wa biashara ikiwemo Canada, Mexico, Umoja wa Ulaya na Japani. Je, Marekani kweli imepata hasara katika biashara na China?

    Mjumbe wa mazungumzo ya biashara ya kimataifa ambaye pia ni naibu waziri wa biashara wa China Bw. Fu Ziying hapa Beijing amesema, tofauti ya idadi ya biashara kati ya Marekani na China haimaanishi hasara au faida. Amesema, katika ushirikiano wa biashara kati ya nchi hizo mbili, , faida zilizopata kampuni za Marekani zimezidi kwa kiasi kikubwa zile zilizopata kampuni za China. Idadi ya bidhaa za China zinazouzwa nchini Marekani inazidi zile za Marekani zilizonunuliwa na China.

    Ukweli wa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili ni kwamba, Marekani imepata faida kubwa zaidi, na kutokana na maendeleo ya miaka 40, kampuni za nchi hizo mbili zimeungana na kutegemeana. Thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imefikia dola bilioni 700 za kimarekani, mapato ya kampuni za Marekani yanayotokana na mauzo ya bidhaa nchini China pia yamefikia dola bilioni 700 za kimarekani, huku faida zao zikizidi dola bilioni 50 za kimarekani.

    China na Marekani ziko sehemu tofauti za mnyororo wa uzalishaji na thamani, yaani Marekani iko kiwango cha juu huku China ikiwa kiwango cha chini. Faida za kampuni za China zinatokana na gharama ya utengenezaji, lakini kampuni za Marekani zimepata faida kubwa katika ubunifu wa bidhaa, utoaji wa vifaa na mauzo ya bidhaa. Kwa mfano simu ya mkononi ya kisasa ya chapa ya Apple inayobuniwa nchini Marekani, inatengenezwa nchini China na kuuzwa duniani kote. Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2018 iliyotolewa na kampuni ya Goldman Sachs ya Marekani, kama kampuni ya Apple ikihamisha viwanda vya simu hiyo nchini Marekani, gharama ya utengenezaji wa simu hiyo itaongezeka kwa asilimia 37.

    Kwa upande wa matumizi, bidhaa nyingi za China zenye bei nafuu na sifa nzuri zinaingia katika familia za Marekani, kuboresha maisha ya wamarekani na kupunguza gharama za maisha. Utafiti wa kamati ya biashara ya taifa ya Marekani umeonesha kuwa, mwaka 2015 biashara kati ya China na Marekani ilipunguza gharama ya matumizi ya kila familia kwa dola 850 za kimarekani.

    Hivyo, ukweli wa biashara huria ni kuwa upande mmoja unanunua kwa hiari huku upande mwingine ukiuza kwa hiari. Marekani inanunua bidhaa kutoka China kutokana na mahitaji ya soko lake wala sio kulazimishwa na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako