• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Iran alaumu vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi yake kuwa ni ugaidi wa kiuchumi.

    (GMT+08:00) 2018-09-26 09:19:54

    Rais wa Iran Hassan Rouhani amelaumu vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi yake kuwa ni ugaidi wa kiuchuni.

    Lawama hizo amezitoa kwenye mjadala unaoendelea wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Amesema usalama duniani upo hatarini kutokana na baadhi ya nchi kudharau na kupuuza thamani ya kimataifa na taasisi. Amesisitiza kuwa kupambana na ushiriki wa pande nyingi sio ujasiri bali ni dalili ya udhaifu wa kiakili.

    Aidha Bw. Rouhan amemlaumu rais Donald Trump wa Marekani kwenye hotuba yake, akisema anataka kupindua utawala wa Iran. Hata hivyo amesema wameridhishwa na jumuiya ya kimatafa kwa kutofurahia kitendo cha Marekani kujitoa kinyume cha sheria kwenye makubaliano ya nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako