• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yakamata watu 22 wanaohusishwa na shambulizi kwenye gwaride la kijeshi

    (GMT+08:00) 2018-09-26 09:50:55

    Habari kutoka gazeti la Tehran Times zinasema kuwa, wizara ya ujasusi ya Iran jana iliwakamata watu 22 wanaohusishwa na shambulizi kwenye gwaride la kijeshi mjini Ahvaz.

    Habari zinasema, silaha, vifaa vya mlipuko na vifaa vya mawasiliano vimekamatwa kutoka watu wanaohusishwa na shambulizi hilo.

    Habari nyingine kutoka shirika la habari la Tasnim zinasema kuwa, hakuna taarifa za kina kuhusu kukamatwa kwa watu hao na kuthibitishwa kwa watuhumiwa, lakini wizara ya ujasusi inasema magaidi wamefadhiliwa na baadhi ya nchi za kiarabu.

    Wizara hiyo inasema, kulikuwa na magaidi watano kwenye shambulizi hilo, wawili kati yao wameuawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako